• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday 31 January 2018

    Magufuli aihaidi bilioni 10 idara ya uhamiaji

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameahidi kutoa pesa za kitanzania jumla ya Bilioni 10 Kwa Idara ya Uamiaji nchini ili kuboresha makao makuu ya idara hiyo.
    Akizungumza leo katika uzinduzi wa Pasi za kusafiria za mfumo wa kielektroniki, Rais Magufuli amesema kwamba ameamua kutoa pesa hizo kutokana na uzalendo unaooneshwa na Idara hiyo.
    Rais Magufuli amesema kuwa kutokana na jinsi idara hiyo inavyojitahidi kufanya kazi kwa juhudi kubwa ndiyo maana aliamua kuwapatia nyumba  103  mkoani Dodoma ambapo serikali imewahamishia makazi yake na kuongeza kuwa ni taasisi ya kwanza kupatiwa nyumba katika mji huo.
    "Dkt. Makakala Katafute eneo, nitawapa bilioni 10 wakati wowote mutakapozihitaji muanze kujenga makao makuu ya uhamiaji, na natoa hizi kwa shukrani ya kazi nzuri unayofanya wewe na watendaji wako". Rais Magufuli
    Ameongeza "Hapa jinsi palivyokaa kaa hapafananii na makao makuu ya uhamiaji. Na kwa vile mmekubali kuhamia Dodoma  ni lazima tuwe na jengo zuri litakalokaa kama makao makuu ya Immigration yenye 'parking nzuri hata mtu akitoka huko anajua kwamba anakwenda uhamiaji. Najua kuna baadhi ya wafanyakazi watalaumu kuhama kwa sababu wanajua wanachofanyaga kwenye yale mabanda yale na mbinu zao za kutengeneza michuzi".

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI