Raisi wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa amemtengua Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Butiama Solomon Kamlule Ngillule kutokana na kushindwa kusimamia vyema maeneo yake ya kazi.
Taarifa hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa nchi Selemani Jafo amesema kuwa Mkurugenzi huyo ametenguliwa kufuatia na ziara ya kikazi aliyoifanya Waziri mkuu wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa na kubaini watendaji waliochini katika baadhi ya halmashauri wameshindwa kusimamia vyema maeneo yao ya kazi.
Kutokana na hali hiyo Raisi Magufuli amemwelekeza katibu mkuu,ofisi ya Rais-TAMISEMI kuchukua hatua stahiki Kwa mweka hazina aliyehusika wakati wa matumizi mabaya yaliyofanywa juu ya fedha hizo za serikali.
Aidha Waziri Jafo amewataka watendaji watendaji wote walio chini ya Tawala za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa kufanya kazi Kwa weledi na kuzingatia kanuni za utumishi wa umma na kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kwa maslahi mapana ya wananchi na taifa.
No comments:
Post a Comment