Kesi inayomkabili Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA) Joseph Mbilinyi
'Sugu' na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyassa, Emmanuel Masonga
imeharishwa siku ya leo baada ya kutokea mabishano makali Mahakamani
hapo ya kisheria kutokana na ushahidi uliyotolewa.

Kutokana na hali hiyo Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Mbeya Michael Mteite amehairisha kesi hiyo mpaka siku ya kesho (Jumatano) ambapo atoa uamuzi wa juu ya hilo kama utasikilizwa ushahidi huo wa sauti mbele ya Mahakama au laa.
Mbunge huyo wa Mbeya mjini na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyassa walishikiliwa na jeshi la polisi wakituhumiwa kutenda kosa la uchochezi katika mkutano wao wa hadhara ambao ulifanyika Disemba 31, 2017 jijini Mbeya ambapo jeshi la polisi linasema kuwa viongozi hao walizungumza maneno yenye kuleta chuki kati ya Serikali na wananch
No comments:
Post a Comment