• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday, 23 January 2018

    Babu Seya atahadharishwa

    Mkali wa muziki wa Chakacha na Mduara AT ambaye jana tu ameachia wimbo wake mpya wa 'Kazi yao', ametoa ushauri mzito kwa Babu Seya akimtahadharisha kuhusu kiki.
    Ikiwa ni muda mfupi tu tangu atoke jela, AT anamwambia Babu Seya awe makini sana na watu wanaomzunguka, wanapomshauri juu ya Kiki na matumizi ya mitandao ya kijamii.
    Akipiga Stori na eNEWZ, AT amesema kuna watu wengi ambao watakuwa hawapendi kumuona Babu Seya na mwanae wakifanikiwa katika maisha jambo ambalo linaweza kupelekea wao kushindwa kutumia vizuri mitandao ya kijamii hasa katika kuhakikisha wanasapoti kazi zao.
    Hata hivyo AT amesema kwamba yeye alipata shida sana haswa pale alipoanza kusikiliza maneno na ushauri wa mashabiki hali iliyopelekea mpaka akabadilisha aina ya mziki ambao alikuwa anaufanya na kuhamia katika Bongo fleva kitu ambacho anaamini kwamba kilimrudisha nyuma kisanaa.
    Kwa upande wa mziki wake AT amesema ameamua kujikita rasmi katika mziki wa mduara mpaka ahakikishe anarudisha heshima ya jina lake ambalo anaona linapotea na kipindi hiki hatosikiliza ushauri wa mtu yeyote ambaye atamshauri kinyume na mipango yake.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI