• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday, 23 January 2018

    Mwigulu Nchemba amvaa Nabii Tito

    Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba ameagiza kukamatwa na kupimwa akili mtu anayejiita Nabii Tito na kuchunguzwa na endapo itabainika kuwa ni mtu mwenye akili timamu kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
    Mwigulu Nchemba amesema hayo akiwa jijini Dar es Salaam kwenye Kanisa la Wasabato Mburahati kwenye harambee ya ujenzi wa kanisa hilo na kusema kuwa watu wa namna hiyo wanaleta chuki na kama wakiachwa wanaweza kuhatarisha hali ya amani ya nchi.
    "Nchi yetu hii tunaishi kwa kuheshimiana kwasababu tunaheshimu imani za watu ndio mana mpaka sasa bado tupo pamoja, wewe kama unajua wakristu wanaamini kama hakutakuwepo kanisa lipo kama baa au danguro wewe unaamua kutengeneza  kanisa la aina hiyo au ndugu zetu waislam wao hawaamini katika Kitimoto wewe unaanzisha Msikiti ambao ukiingia tu unapewa Kitimoto huko ni kutengeneza chuki, uchochezi ambao unaweza kuleta uvunjifu wa amani" Mwigulu Nchemba

    "Mtu huyu kwa sababu ni mtu mzima kwanza akamatwe apimwe akili vizuri na kama yupo sawasawa basi afike kwenye vyombo vya sheria, hauwezi kututengenezea vitu ambavyo vinaweza kuleta mapigano ya imani ndani ya nchi yetu, vita ya kiimani haina mshindi kwani mtu kwenye imani yake yupo tayari kufa, kama ni mgonjwa basi akatibiwe

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI