• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday, 23 January 2018

    Kenya yatengeneza setilaiti yake ya kwanza


     Setlaiti

    Kenya imetengeneza setilaiti yake ya kwanzkabisa ambayo imepangiwa kurushwa anga za juu Machi mwaka huu.
    Wahandisi kutoka chuo kikuu cha Nairobi, wakisaidiwa na maafisa kutoka shirika la anga za juu la Japan walitenengeza chombo hicho katika mradi uliogharimu zaidi ya dola milioni moja.
    Setlaiti hiyo itatumika kuchunguza mienendo ya kilimo, pamoja na kuchunguza maeneo ya pwani ya taifa hilo.
    Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo anasema setilaiti hiyo ni ya umbo la mchemraba na ina ukubwa wa sentimita 10 mraba - hujulikana kama nano-setilait
    Japan ilitoa ufadhili na jukwaa la kuitengenezea lakini ni Wakenya wenyewe walioitengeneza.
    Setlaiti hiyo itatumwa hadi Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS) mnamo mwezi Machi na kuzinduliwa rasmi kuizungukza dunia na roboti mwezi mmoja baadaye.
    Hatua hiyo itaifanya Kenya kuwa miongoni mwa mataifa mengine saba barani Afrika yaliyo na setilaiti zinazoizunguka dunia.
    Mataifa mengine ni Misri, Afrika Kusini, Morocco, Algeria, Nigeria, Mauritius na Ghana.
    Kundi la wahandisi kutoka chuo kikuu cha Nairobi walioitengeza walikuwa kundi la kwanza kufaidika kutokana na mradi wa pamoja kati ya Umoja wa Mataifa na shirila la anga za juu la Japan unaolenga kuzisaidia taasisi za elimu kutoka mataifa yanayostawi kutengeneza setilaiti zao.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI