Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt John Pombe Magufuli Ni kuitaka tanzania ya Viwanda ambapo Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda leo amekutana na ugeni wa wawekezaji kutoka China kujadilia na kuhusu mambo ya uwekezaji.
Akizungumza katika mkutano huo Mhe. Makonda amesema kutokana na malengo yaliyo we kwa na Wizara ya TAMISEMI maelekezo kutoka kwa Rais John Pombe Magufuli kuwa kila mkoa uhakikishe unaenda viwanda 100.
Wawekezaji hawa wanakwenda kuwekeza Tanga na kunduchi Dar es Salaam na Wana wekeza miradi yenye thamani ya Dola bilioni 3dola.
Aidha amewataka wanachi wa mkoa huo kuchangamkia fursa za uwekezaji
"sisi kazi yetu kama serikali ni kuweka mazingira ya uwekezaji na hawandugu zetu wametoka jimbo la nilizungumza nao nilipotembelea huko kwao mwakajana"Amesema Makonda.
Pamoja na hayo Makonda Kuna clip ina zungunguka mtandaoni ikieleza kuwa Ethiopia kuwa Wana kiwanda kikubwa zaidi kuliko nchi zote barani Afrika na kusema kuwa wananchi wasihofu kwani Dar es Salaam itajenga kiwanda kikubwa zaidi ya mara tatu ya hicho chenye Siguare mita Milion Tano na uwekezaji huu utafanyika wilayani Kigamboni.
"Kuna mwekezaji mwingi ameonyesha nia ya kuwekeza kiwanda cha sukari Nawaomba wafanyabiashara wetu mchangamkie fursa hizo za kibiashara na vijana pia mchangamkie fursa za ajira" Amesema Makonda.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa jimbo la Gwangzou , Xie zhenghy kutoka China amesema wao wako tayari kwa uwekezaji na katika nchi ambazo zitaendana kiutamaduni kama ilivyo kwa Tanzania.
Hata hivyo amesema kuwa China imekuwa na nafasi kubwa ya kuwekeza barani Afrika ambapo imekuwa na uwekezaji mkubwa nchini Misri.
Akizungumzia uwekezaji hapanchini amesema kuwa uwekezaji watakaofanya ni ule unaendana na kaulimbiu ya Rais John Pombe Magufuli.
No comments:
Post a Comment