Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amewabadilikia baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya awamu ya tano na
kuwataka kutenda kazi kama atakavyo yeye kwani wasipofanya hivyo maana
yake nafasi hizo haziwafai tena.
Magufuli amesema hayo leo wakati wa sherehe za kuapishwa kwa Naibu
Waziri wa Madini, Doto Mashaka Biteko leo Ikulu jijini Dar es Salaam na
kudai kuwa haridhishwi na utendaji kazi wa Waziri wa Madini, Anjellah
Kairuki pamoja na Naibu wake Stanslaus Nyongo na kuwataka kubadilika
mara moja.
"Bado Wizara ya Madini haifanya kazi vizuri sana najua
nikizungumza kwa kupamba nitakuwa mnafiki Mhe. Spika utatambua mwezi wa 7
Bunge lilipitisha sheria ya madini kubadilisha ile sheria iliyokuwepo
mkapitisha sheria namba 7 ya mwaka 2017 ambayo Bunge na Watanzania wengi
tuliamini kwamba kupitia sheria hii mambo mengi ya nchi yangenyooka
ikiwa pamoja na kupata mlahaba na kupata faida na madini yetu. Ile
sheria ilipofika nilisaini na kuwapa maelekezo watendaji wangu kuandaa
'regulations' lakini mpaka sasa ni miezi saba imepita regulations
hazijasainiwa" alisema Rais
Rais Magufuli aliendelea kusisitiza kuwa kutokana na vitendo hivyo
vya wateule wake ni wazi kuwa kuna matatizo makubwa ndani ya Serikali
"Unaweza kujiuliza kuwa tuna matatizo makubwa ndani ya
Serikali, kwa sababu kama regulations zile hazijasaini mnategemea nini?
Kuanzia mwezi wa saba hawakusaini leo tupo mwezi wa kwanza bado
hazijasainiwa, usipokuwa na regulations mtu yoyote atakapo default
atapelekwa kwenye mahakama gani? Kwa hiyo sisi Watanzania baadhi ya
watendaji wa Serikali hawapo makini ninasema hii kwa uchungu mkubwa
baadhi ya niliowateua bado hawajanielewa ninataka nini" alisisitiza Rais
Pia Rais Magufuli alitumia nafasi hiyo kutuma ujumbe kwa Waziri wa Madini, Angellah Kairuki ambaye sasa yupo likizo "unapokuja
kukumbushwa kwamba kuna haya mabaya kwenye eneo lako na wewe upo maana
yake ni kwamba hufiti, unatakiwa wewe uyagundue kabla ya watu wengine
kuyagundua kwa hiyo Wizara ya Nishati mnachangamoto kubwa bado mengi
hayajafanyika. Wizara ya Madini mkajirekebishe mfanye kazi kiukweli
mpaka sasa Wizara ya Madini haija ni 'impress' na mumfikishie salamu
hizi waziri bado haja ni 'impress' lakini nategemea mtabadilika" alisisitiza Rais

No comments:
Post a Comment