Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Januari 16, 2018 amepokea hati za
utambulisho wa Mabalozi sita walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa
nchini na kuwaomba mabalozi hao kuwakaribisha viongozi wa nchini zao
kutembelea Tanzania.

Taarifa
iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa
imesema kuwa mabalozi hao waliowasilisha hati za utambulisho ni pamoja
na Balozi wa Nigeria hapa nchini, Balozi wa Polanda, Balozi wa Uturuki,
Balozi wa Ufaransa, Balozi wa Israel pamoja na Balozi wa Australia.


No comments:
Post a Comment