Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam imetenga takribani shilingi
bilioni moja na milioni mia moja, kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vijana
na wanawake.

Aidha Bi. Andrew ameongeza kuwa mikopo hiyo itaanza kutoka hivi karibuni na kuwataka wakazi wa Ubungo wachangamkie fursa hiyo inayotokana na ahadi ya serikali ya kuwawezesha wananchi wake kiuchumi.
Kwa upande mwingine Bi. Andrew amesema tayari fomu za maombi ya mikopo hiyo zimeshapelekwa kwa maofisa maendeleo ya jamii kwenye kata zote 18 za Manispaa hiyo.
Afisa maendeleo huyo amemaliza kwa kusema kuwa kipaumbele katika kupata mikopo hiyo kitatolewa kwenye biashara zinazofanywa kwenye maeneo rasmi
No comments:
Post a Comment