Na Stahmili Mohammed.
Mkutano
mkuu wa chama cha maafisa habari Na mawasliano serikalini (TAGCO) kwa
kushirikiana na idara ya habari maelezo habari, utamaduni na michezo
unatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 12-16 machi mwaka huu mkoani Arusha
ambapo jumla ya maofisa 300 wanatarajiwa kishiriki katika mkutano huo.
Akiongea
Na vyombo vya habari leo jijini dar es salaam mwenyekiti wa chama hicho
Paschal Shelutete amesema kuwa lengo kuu kuelekea mkutano huo ni
kuweza kukumbushana wajibu na majukumu yao serikalini.
Aidha
amesema kuwa kikao hiko kina kazi ya kuwajengea washiriki uwezo wa
namna ya kutangaza shughuli za serikali Na kuhakikisha idara ya
mawasikiano Na uhusiano serikalini vinaimarishwa ili kuendana na kasi ya
utendaji wa serikali ya awamu ya tano.
Pia
ameongeza na kusema kuwa katika mkutano huo jumla ya mada 14
zitaongelewa ambazo zitajikita zaidi kwenye masuala mbalimbali yahusuyo
habari, mawasiliano na itifaki.
Pia
amesema kuwa mada hizo zitawasilishwa na wataalam watakaoleta uzoefu
mpana katika mawasiliano na kuongeza kuwa kutakuwepo mijadala na fursa
ya kubadilishana uzoefu kati ya maaafisa mawasiliano na wadau wengine wa
habari.
Mwisho
kabisa amewahasa maafisa habari, mawasiliano, uhusiano na itifaki
kuthibitisha ushiriki wao kabla ya tarehe 7 machi mwaka huu.
No comments:
Post a Comment