Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Solomon Mndeme, ameipa tahadhari mikoa
ya jirani dhidi ya ugonjwa hatari ulioukumba mkoa huo, wa kushambuliwa
kwa mazao na wadudu.

Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv Bi.
Mndeme amesema ni vyema mikoa hiyo ikachukua tahadhari ili
isijeathirika na kupata madhara makubwa kama yao, na kuleta hasara kubwa
kwa jamii.
“Tunawaambia na majirani kwamba wachukue tahadhari wajikinge na ugonjwa huu, tumewaambia maafisa ugani wasikae ofisini waende 'field' kwa wakulima watoe elimu, kwa kweli ni 'disaster', kuhusu wakulima wetu tumewashauri wapande upya kwa sababu bado kuna mvua”, amesema Bi. Mndeme.
Hivi karibuni kumeripotiwa kuwepo kwa uharibifu mkubwa wa mazao ya mahindi, ambapo heka 82 za wakulima wilayani Songea zimeharibiwa na wadudu.
CHANZO EATV.

No comments:
Post a Comment