Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani) baada ya
kuwasili kwenye kambi ya Uvuvi ya Kisiwa cha Galinzila leo na kuongea na
wavuvi. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Estomiah Chang’a (mwenye
kofia) na kulia zaidi ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ukerewe
Frank Bahati leo. Mhe. Mpina alichoma moto nyavu haramu za uvuvi
zenye thamani ya shilingi bilioni mbili. (Na John Mapepele)
zenye thamani ya shilingi bilioni mbili. (Na John Mapepele)
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani) akiwahutubia
wavuvi kwenye kambi ya wavuvi katika kisiwa cha Galinzila Wilayani
Ukerewe ambapo baadaye alichoma moto nyavu haramu za
uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni mbili katika kijiji Kakukuru. (Na John Mapepele)
uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni mbili katika kijiji Kakukuru. (Na John Mapepele)
Umati wa wavuvi kwenye kambi ya wavuvi ya Kisiwa cha Galinzila wilayani Ukerewe wakimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (hayupo pichani) ambapo baadaye alichoma moto nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni mbili katika kijiji cha Kakukuru zilizokamatwa katika operesheni maalum ya siku tanoya kutokomeza uvuvi haramu katika Wilaya ya Ukerewe leo
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi,
Mhe Luhaga Mpina ametaifisha na kuteketeza zana haramu za uvuvi zenye
thamani ya shilingi bilioni 2 zilizokamatwa wakati zikitumika kwa
shughuli za uvuvi katika visiwa vidogo vilivyopo ndani ya Wilaya ya
Ukerewe mkoani Mwanza huku Shilingi milioni 120 zikikusanywa kama sehemu
ya adhabu kwa wavuvi na wafanyabiashara waliokutwa na zana haramu
pamoja na makosa ya utoroshaji samaki na mazao yake nje ya nchi.
Waziri Mpina aliwaonya watu
wanaotumia majina ya wavuvi kutishia kufanya migomo isiyoisha na
kuandamana baada ya uamuzi wa Serikali kuanza kuchukua hatua stahiki za
kudhibiti uvuvi haramu, na kwamba msimamo uliowekwa na Serikali ni
thabiti na usiyoyumba hivyo migomo na maandamano ya watu wenye lengo la
kukwamisha vita dhidi ya uvuvi haramu haitasaidia chochote na badala
yake operesheni kali isiyo na mwisho itaendelea hadi pale uvuvi haramu
utakapokoma ndani ya Ziwa Victoria.
“Rasilimali zilizopo ndani
ya ziwa hili ni mali ya wananchi sisi viongozi mliotupa dhamana ya
kuongoza kazi yetu ni ulinzi tu na endapo tutakomesha uvuvi haramu nyie
ndio mtakaonufaika hivyo ni itashangaza tajiri aliyempa kibarua cha
ulinzi, na mlinzi huyo akafanya kazi vizuri ya kulinda mali za bosi wake
alafu tajiri akamlalamikia kibarua wake sisi na watendaji wa Serikali
ni vibarua tu wenye mali ni ninyi hatua tunazochukua zitaleta manufaa
makubwa kwenu”alisema.
Pamoja na kuteketeza zana
haramu, Waziri Mpina alieleza hali ya upatikanaji wa samaki aina ya
sangara katika Ziwa Victoria ambapo alisema kwa mujibu wa utafiti
uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Samaki Tanzania (TAFIRI) 2017
unaonesha kuwa samaki waliochini ya sentimita 50 ni asilimia 96.6 hivyo
samaki hawa ni wachanga na hawarusiwi kuvuliwa ambapo samaki walio
zaidi ya sentimita 85 ni asilimia 0.4 tu ambao ni wazazi na hawarusiwi
kuvuliwa pia. Samaki wa sentimita 50 mpaka 85 ambao ndio wanafaa
kuvuliwa ni asilimia 3 tu.
kuvuliwa ni asilimia 3 tu.
“Tafsiri yake ni kwamba ziwa halina samaki wanaostahili kuvuliwa kulingana na kasi ya uvuvi na pia samaki
wazazi ni kidogo ambapo inatishia kumalizika kwa samaki na shughuli za uvuvi kukoma katika Ziwa Victoria’alisema .
wazazi ni kidogo ambapo inatishia kumalizika kwa samaki na shughuli za uvuvi kukoma katika Ziwa Victoria’alisema .
Akizungumza kwa nyakati
tofauti na maelfu ya wavuvi katika Visiwa vya Gagalini na Kakukuru
wilayani Ukerewe Waziri Mpina amesema hatua kali zinazochukuliwa na
Serikali dhidi ya uvuvi haramu hazilengi kuwaonea wananchi wanyonge bali
kuwatengenezea maisha bora ya kizazi cha sasa na baadae ili kiweze
kunufaika na rasilimali zilizoko ziwani.
Akiwa katika eneo la Kakukuru
Waziri Mpina alishiriki kuteketeza zana haramu zikiwemo vyavu za Makila
14,103, Kokoro 188 , Nyavu za dagaa 211, Nyavu za timba 450, Kamba za
Kokoro 10,700 na ndoano 18,450 na Mitumbwi 109 zenye thamani ya sh.
Bilioni 2.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo
ya Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mwaidi Mlolwa amesema Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha 26 (i) (ii) kinamtaka kila
mtanzania kulinda rasilimali
za nchi yetu ikiwemo samaki na mazao yake huku Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2009 zikikataza vitendo vya kutumia zana zisizoruhisiwa kwa mujibu wa sheria.
za nchi yetu ikiwemo samaki na mazao yake huku Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2009 zikikataza vitendo vya kutumia zana zisizoruhisiwa kwa mujibu wa sheria.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe,
Estomihn Chang’a alisema Serikali ya wilaya hiyo itaendelea kuunga mkono
juhudi za kupambana na uvuvi haramu na kuwachukulia hatua stahiki
kuwataka wananchi kuendelea kuwafichua wavuvi haramu ili kulinda
rasimali hiyo muhimu waliyopewa na Mungu.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Ukerewe , Frank Bahati alisema halmashauri imewasimamisha kazi watumishi
watatu kwa tuhuma za kujihusisha na uvuvi haramu.
Kwa upande wao baadhi ya
wavuvi walimuomba Waziri Mpina kuwasiliana na Waziri wa Viwanda na
Biashara, Charles Mwijage ili kuona namna ya kudhibiti nyavu
zisizoruhusiwa kutengenezwa na kisha kuuziwa wavuvi
No comments:
Post a Comment