• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 15 January 2018

    RC MAKONDA AMALIZA MGOGORO WA MAMA ALIETAPELIWA NA MCHUNGAJI

    Image result for makonda
    Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda leo amemsaidia Mama Mjane Bi.Benadetha Rwendela aliedhulumiwa Nyumba yake Plot No. 239 Block B Kunduchi Beach kwa kupigwa Mnada na Madalali kutoka Kampuni ya Nkanya Ltd kinyume na taratibu kisha kuamrishwa kuondoka ndani ya siku 30.
    Baada ya RC Makonda kuona taarifa hizo kwenye baadhi ya Vyombo vya Habari na Mitandao alimwita Mjane huyo Ofisini kwake kisha kumkutanisha na Wanasheria wa Mkoa na kubaini utapeli uliotumika kuuza
    Nyumba hiyo kutokana na watu kufoji nyaraka ikiwemo Sahihi ya Mwenyekiti wa Mtaa huku nyumba hiyo ikiwa Zuio la Mahakama.
    Aidha imebainika Kuwa Hati za Nyumba hiyo zilifojiwa kisha kutumika kuchukuwa Mkopo wa Shilingi Billion Moja pasipo mmiliki wa nyumba kujua kinachoendelea.
    Kutokana na hilo RC Makonda ameagiza Kamanda wa Polis Kanda Maalumu ya Dar es Salaam LAZARO MAMBOSASA kuwakamata Matapeli waliohusika pamoja  kuagiza kusimamishwa Mnada huo kwakuwa ni batili  huku akimsihi Mama Mjane  kuishi kwa Amani kwenye nyumba yake.
    Aidha RC Makonda amesema Jumatatu ya wiki ijayo atakutana na Bank ya KCB kwaajili ya Mazungumzo huku akiwaagiza Madalali wote wanaotaka kufanya minada kwenye Mkoa huu kuhakikisha wanapata ruhusa kutoka kwa Wakuu wa Wilaya.
    Kwa upande wake Mjane huyo Bi. Benadetha Rwendela ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuwajali Wananchi wake na kuwasaidia pale wanapopata matatizo huku akimpongeza Rais Magufuli kwa kumteua RC Makonda.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI