Jeshi la polisi nchini limewataka wahalifu wote waachane na dhana ya uhalifu kwani atakayebaika hatasalimika.
Amesema hayo IGP Simon Sirro leo wakati wakisaini mkataba
wa makubaliano wa kufanya kazi kwa kushirikiana kwa lengo la kutokomeza
uhalifu ila kuhakikisha raia wa msumbiji na Tanzania wako salama.
Pia amesema wahalifu wote wanaoendelea kufanya vitendo vya
kiuhalifu waache mara moja kwani wanaweka maisha yao hatarini pindi
jeshi litakapowashika.
Kwa upande wa IGP wa Msumbiji Bernadino Raphael amesema
makubaliano hayo ya kupambana na jeshi uhalifu kati ya hizi nchi mbili
itasaidia watu kuishi kwa amani na wanategemea kuzidi kuimarisha ulinzi
zaidi kwenye mipaka ya nchi hizi mbili ili waweze kuwakamata kiurahisi
wahalifu wanaotenda makosa na kukimbilia nchi jirani.
No comments:
Post a Comment