Kampuni ya reli Tanzania(TRL)imeamua
kuendelea kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria kuanziaDodoma kwenda
kigoma,mwanza na Mpanda hadi hali ya miundombinu itakapokuwa vizuri
baada ya ukarabati kukamilika.

Hayo
yamesemwa Leo na Kaimu Naibu Mkurugenzi wa TRL Focus Makoye Saloni
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mabadiliko ya
safari za treni Mara baada ya kuharibiwa kwa miundombinu ya reli ya
kati ya Stesheni za kilosa na Gulwe kutokana na mafuriko ya mvua
zilizonyesha maeneo hayo.
Akitaja
ratiba ya usafiri huo kuanzia Dodoma na muda wa safari Bw.Makoye
amesema treni itaanza safari Dodoma itatoka Saa moja usiku Sikh ya
jumanne na ijumaa kwenda kigoma Mpanda na kuwasili mwanza saa 12 jioni
siku ya jumatano na mpanda sa 12:00 jioni na kigoma saa 12:30 jioni.
Aidha
Treni kutoka Mpanda ,mwanza na kigoma zitatoka huko siku za jumapili na
alhamisi tu.Treni hiyo itatoka saa 1:00 asubuhi mwanza inatoka saa 2:00
asubuhi na kigoma inatoka saa 1:30 asubuhi hivyo treni hizo zinafiks
Dodoma siku ya jumatatu na ijumaa saa 1:00 asubuhi.wakati huo huo treni
pekee ya kutoka Tabora kwenda Mpanda itafanya safari zake siku ya
jumanne,Alhamisi na jumapili na itatoka Mpanda kurejea Tabora katika
siku za jumatatu,jumatano,jumamosi na itakuwa ikiondoka Tabora saa 12
asubuhi na kuwasili Mpanda saa 12:32 jioni na itaondoka Mpanda kurejea
Tabora saa 1:00 asubuhi na kuwasili saa 12:38 jioni.

Kwa
upande wake Meneja wa usalama wa reli Gakwi Michael amesema tabia ya
watu kulima pembezoni mwa reli wamechangia kwa kiasi kikubwa hivyo
amewataka watu kwenye Tania hizo kuacha Mara moja.
Hata hivyo uongozi wa TRL bado unaendelea kusimamia kazi ya ukarabati wa eneo lililoharibika kati ya kilosa na Gulwe.
No comments:
Post a Comment