• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 25 January 2018

    Mwanafunzi abakwa na kuuawa kikatili

    Mwanafunzi wa kike wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 14 mkoani Katavi, ameuawa kikatili baada ya kubakwa na kuchomwa kisu, na kisha mwili wake kutelekezwa porini na mtu ambaye alimpa lifti.
    Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Damas Nyanda, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba imetokea wakati binti huyo akienda shule akiwa na mdoo wake wa kiume, na njiani kuomba lifti ya mtu ambaye walikuwa hawamfahamu, ambaye anasadikiwa kufanya tukio hilo la kukataisha uhai wake.
    Kamanda Nyanda ameendelea kueleza kwamba baada ya binti huyo kuomba lifti alipewa lifti hiyo, na kumuacha mdogo wake akiwakimbilia bila mafanikio, na ndipo inasadikiwa kuenda kuuliwa.
    “Ni kwweli tukio hilo limetokea, ni binti mdogo wa miaka 14 mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Vikonge, alikuwa ameongozana na mdogo wake wa kiume wakielekea shuleni, njiani yule binti aliomba lifti ya pikipiki, yule dereva boda boda alimchukua na kumuacha mdogo wake,  yule mtu aliendesha ile pikipiki kwa kasi isiyo ya kawaida huku mdogo mtu akiikimbilia bila mafanikio”, amesema Kamanda Nyanda.
    Kamanda Nyanda ameendelea kuelezea kuwa ...”Ghafla aliiona pikipiki ile iliyombeba dada yake ikiwa imeegeshwa karibu na kichaka kando ya barabara inayoelekea shuleni kwao na akaipita. Bila shaka kutokana na umri wake kuwa bado mdogo baada ya kufika shuleni hakushughulika kumtafuta dada yake, aliingia darasani na kuendelea na masomo kama kawaida na baada ya muda wa masomo yaani saa nane na nusu alianza safari ya kurejea nyumbani bila kumtafuta dada yake, aliporudi nyumbani alipoulizwa dada yako yuko wapi, akasimulia tukio lote na wazazi wakiwa na majirani kuamua kufuatilia hapo mahali, na ndipo walipokuta mwili wa binti huyo ukiwa kichakani huku anaonekana amebakwa na majeraha ya visu”, amesema Kamanda Nyanda.
    Jeshi la Polisi mkoani Katavi linaendelea na msako wa mtu aliyefanya mauaji hayo, ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.CHAMZO EATV

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI