Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC) imesema uchaguzi mdogo katika
majimbo ya Siha - Kilimanjaro, Kinondoni mkoani Dar es Salaam na Kata
nne za Tanzania Bara utafanyika Feb 17, 2018 kufutia waliokuwa wabunge
katika majimbo hayo kujivua uanachama.
Taarifa ya Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar,
Hamid Mahmod Hamid, imeeleza kuwa pamoja na majimbo hayo, pia Kata nne
za Isamilo , Manzase, Madanga ndizo zitafanya Uchaguzi mdogo
Aidha, Jaji Hamid amesema, Tume inaendesha uchaguzi huo baada ya
kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Job
Ndugai kuhusu kuwepo wazi kwa jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam na
jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro.
Amesema, barua hiyo ilieleza kuwa majimbo hayo yapo wazi baada Maulid
Mtulia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kujivua uanachama wa CUF
na Dk. Godwin Mollel wa jimbo la Siha kujiuzulu uanachama wa CHADEMA na
hivyo wote kukosa sifa za kuendelea kuwa wabunge.
Pia, ameeleza kuwa Tume ilipokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye
dhamana ya Serikali za Mitaa ikiitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za
Udiwani katika kata nne za Tanzania Bara.
Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la viongozi kuhama vyama vyao vya
siasa na kuhamia vyama vingine hali ambayo serikali inalazimika kuandaa
chaguzi nyingine ili kujaza nafasi zinazoachwa wazi. Uchaguzi wa mwisho
wa marudio ulifanyika Nov 26, 2017 huku mwingine ukitarajiwa kufanyika
Januari 13 mwaka
No comments:
Post a Comment