
Uchaguzi
wa kumpata naibu Meya wa jiji la dar es salaam umefanyika Leo Mara
baada ya jiji hilo kukaa pasipo kuwa na naibu meya takribani miezi sita.
wagombea
katika uchaguzi huo walikuwa ni Marian Ruida kutoka chama cha mapinduzi
na Musa Khafana kutoka chama cha CUF ambapo katika idadi ya kura
zilizopigwa na washiriki wa uchaguzi huo ni 22 huku kura 12
zilinyakuliwa na Mussa Khafana wa CUF na kura 10 zikiwa zimesalia kwa
Mariam Ruida kutokea ccm.
Hata
hivyo Mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo ya uchaguzi mgombea
kutokea ccm mhe.Mariam Ruida aliwashukuru wapiga kura na kuahidi
kushirikiana na uongozi uliopo madarakani .
Naye
Said Kubenea akizungumza kwa niaba ya mgombea wa CUF ambaye hali yake
ya kiafya si nzuri amesema wao kama Ukawa wanashukuru mungu kushinda
nafasi hiyo licha ya kuwa mgombea wao hakuwa katika hali iliyopelekea
wao kupitia changamoto mbalimbali hadi kufikia tamati ya uchaguzi.
No comments:
Post a Comment