• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday, 2 January 2018

    Edmund Mndolwa ahaidi kuimarisha jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi

    Image result for edmund  mwenyekiti jumuiya wazazi taifa
    Na Stahmil Mohamed
    Uongozi mpya Wa Jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi imeahidi kuimarisha umoja Wa jumuiya hiyo na kuifanya ya kujitegemea ili kufikia malengo ya jumuiya pamoja na nchi ya malengo ya uchumi Wa kati ambayo ni Sera ya serikali ya awamu ya tano Jamuhuri ya muungano Wa Tanzania ya Tanzania ya  viwanda.
    Hayo yamesemwa na Mwenyekiti Mpya Wa Jumuiya hiyo DKT Edmund B Mndolwa baada ya kukabidhiwa rasmi Ofisi Leo na aliyekuwa mwenyekiti Wa jumuiya hiyo ambaye kwasasa amemaliza mda wake DKT Abdallah Bulembo ambapo DKT Mndolwa alianza Kwa kumshukuru Dkt Bulembo Kwa kumkabidhi Ofisi rasmi Kwa maandishi na taratibu zote stahiki  ambapo amesema jambo hilo ni nadra sana kuona kwenye taasisi nyingine hivyo hana budi kumshukuru Kwa ujasiri na uzingatiwaji wake Wa sheria kwani anaamini jumuiya ya wazazi ni ya kwanza katika  makabidhiano hayo .
    Aidha DKT Mndolwa  amesema atahakikisha  anaimarisha umoja Wa jumuiya hiyo ili izidi kuleta tija katika jamii pia  atahakikisha jumuiya inakuwa ya kujitegemea zaidi ili kufikia malengo ya Jumuiya na kuepukana na hali ya kuombaomba katika chama ameongeza Kwa kusema kuwa atahakikisha maadili ya watanzania yanakuwa kama miaka ya nyuma ilivokuwa kama agizo la rais John pombe magufuli alivyoagiza kwenye alipokuwa katika mkutano Mkuu wa Jumuiya ya wazazi uliofanyika Dodoma hivo atahakikisha waanzia mashuleni kote kuwajenga kimaadili kwani huko ndipo chimbiko la Taifa la Kesho linapoanzia.
    Naye Makamu Mwenyekiti Wa jumuiya hiyo Haidal Haji Abdallah amesema jumuiya itakimbizana na muda ili izidi kukua na kuimarika zaidi
    Kwa upande wake  DKT Bulembo wakati akimkabidhi  Ofisi DKT Mndolwa pamoja na vitendea Kazi vyote ikiwemo katiba ya chama,kanuni ya Jumuiya na baadhi za Mali za jumuiya kama mashule,magari na kadha Wa kadha pia DKT Bulembo ameahidi kushirikiana na uongozi huu mpya pindi watakapohitaji ushirikiano Wa aina yoyote.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI