Msanii wa filamu na mchekeshaji bongo ambaye pia ni kada wa chama cha
Mapinduzi, Steve Mengere maarufu kama Steve Nyerere, ameonyesha nia ya
kugombea ubunge wa jimbo la Kinondoni.

“Wilaya ya Kinondoni unapozungumzia vijana ambao ni 'president' ni Steve Nyerere, ndio maana jimbo la Kinondoni linanisubiri mimi, we pita kila sehemu uliza tu utaambiwa”, amesema Steve Nyerere.
Kutokana na hilo Steve Nyerere hatokuwa msanii wa kwanza kutangaza nia kwa jimbo la Kinondoni, kwani msanii wa muziki wa bongo fleva Khalid Mohamed maarufu kama TID, alishawahi kusikika akisema anakusudia kugombea ubunge wa jimbo hilo
No comments:
Post a Comment