• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday, 2 January 2018

    Rais Magufuli amesikia kilio cha Babu Seya

    Rais  Dkt. John Pombe Magufuli amesikia kilio cha wanamuziki Nguza Vicking alimaarufu kama 'Babu Seya' na mwanaye Francis Nguza ambao walikuwa wakiomba nafasi ya kukutana naye na kumshukuru kwa kuwapa msamaha wa kutoka jela.
    Akiongea baada ya kuonana na Rais Babu Seya anasema sasa amepewa ruhusa kuanza kufanya kazi na kudai kuwa muda wowote Watanzania wakae mkao wa kula kwani ataanza kufanya kazi yake ya muziki.
    "Nimesikia furaha ya kupitiliza kuonana na Rais kwanza alinisamehe kule nimekuja kutoa shukrani zangu kwake na kumuomba aniruhusu kufanya kazi kwa sababu hii ni awamu ya kufanya tu kazi na mimi nitafanya kazi. Kwa sababu nimesharuhusiwa kufanya kazi wanipe muda kidogo nitawatangazia lini nitaanza kuingia jukwaani lakini kuanzia sasa hivi hapa nipo huru kufanya kazi" alisema Babu Seya
    Aidha Mtoto wa Nguza anayefahamika kwa jina la Papii Kocha kwa upande wake amesema baada ya kupata ruksa ya kufanya kazi sasa wanakuja kufanya ukombozi wa muziki wa Dansi nchini kwani kwa muda ambao wamekaa uraiani wamegundua kuwa muziki huo umepoteza umaarufu wake.
    Disemba 9, 2017 katika sherehe za miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara Rais Dkt. John Magufuli alitoa msahama kwa wafungwa mbalimbali wakiwepo wasanii Papii Kocha na baba yake Nguza Vicking ambao walikuwa wakitumikia kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kubaka na kulawiti watoto wadogo Juni 25, 2004.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI