Rais wa Angola João Lourenço, amemfukuza kazi mtoto wa rais wa zamani
wa nchi hiyo José Eduardo dos Santos ambaye alikuwa Mkuu wa mfuko wa
utajiri wa taifa hilo.
Awali Novemba 15, Rais huyo alimfukuza kazi binti mkubwa wa rais huo wa zamani, Bi Isabel dos Santos kama mkuu wa kampuni ya mafuta ya serikali ya nchi ya Sonangol.
Aidha Rais huyo amemteuwa Waziri wa Zamani wa Fedha kuwa mwenyekiti wa bodi ya mfuko huo (FSDEA) Carlos Alberto Lopes.
Mfuko huo umekuwa ukitajwa sana kufuatia tuhuma zilizovujishwa na gazeti la Paradise kwamba ulilipa fedha nyingi mamilioni ya dola ikiwa na malipo ya ada kwa mfanyabiashara ambaye anafanya kazi kwa karibu na José Filomeno.
No comments:
Post a Comment