• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 11 January 2018

    Wanafunzi wanaojitolea kufundisha waomba msaada

    Na Apolonia Kisite
    Wanafunzi wa chuo cha DUCE wanaojitolea kufundisha katika shule mbalimbali za sekondari za Temeke  wanaomba wadau,taasisi na makampuni mbalimbali kujitokeza kuwawezesha pesa za nauli kusudi waweze kuzifikia shule ambazo ziko mbali na chuo chao.

    Akizungumza na waandishi wa habari Mwanzilishi na mratibu mkuu wa zoezi hilo Mr.Emijidius Cornel amesema mpaka sasa wameweza kuzifikia shule kumi na bado wanania ya kuzifikia shule nyingine kwa ajili ya kujitolea kusaidia wanafunzi wengine zaidi.

     Aidha amesema kwa huu 2018 wametanua wigo na kujitolea kwenye shule za msingi za Temeke kusudi waweze kuwajengea uwezo wanafunzi hasa wakiwa bado wadogo kuyapenda,kuyasoma na kuyapa kipaumbele masomo ya sayansi na hesabu.

     Pia amesema ili waendelee kufikia lengo wanamuomba raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli azidi kuwapa ushirikiano na kuweza kuwatembelea katika chuo chao DUCE.

    Sambamba na hayo anawashauri wanafunzi wenzao walio kwenye vyuo mbalimbali nchini Tanzania kuwa na tabia ya kujitolea kufanya shughuli mbalimbali zenye lengo la kuleta maendeleo kwenye jamii yetu ya Tanzania.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI