Mamlaka ya udhibiti usafiri barabarani (SUMATRA) wamekutana na chama cha wamiliki mabasi yaendayo mkoani (TABOA) na abiria kujadili na kuchambua kanuni mpya za leseni za usafirishaji na baadhi ya kanuni zilizorekebishwa.
Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi wa udhibiti wa usafiri barabarani (SUMATRA) Johansen Kahatano amesema lengo la mkutano huu ni kuzichambua kanuni hizo na kuelimishana pia ni muhimu kila mwaka kukutana na wadau hao ambao ni madereva,wamiliki wa mabasi na abiria ili kuwaelimisha na kufahamu haki na sheria zinazowaongoza brabarani ili kusaidia kuepuka ajali zisizokuwa na lazima.
Pia aliongezea kwa kusema kwa abiria wanaosafiri kwenda mikoani wafahamu haki zao kwani endapo wakiwa wanataka kusafiri na madereva kuchelewesha gari kuanza safari ikiwa tiketi inaonesha muda wa kuondoka umepita zaidi ya saa moja inawapasa kutoa taarifa kwa mamlaka husika ili kuwapa adhabu na kutatua tatizo hilo lisiwe endelevu.
kwa upande wa mjmbe wa chama cha mabasi yaendayo mkoani(TAMOBA) Mwesigwa kazaula amesema kuna mvutano mkubwa uliopo kati yao na mamlaka hiyo kuhusiana na tozo ya faini ya laki mbili kwa kila kosa bila kuangalia ukubwa wa kosa hilo kwani inawaumiza kwa kiasi kikubwa kwa upande wao ikiwa hawana faida kubwa wanayopata katika mabasi hayo.
Aidha mjumbe huyo ameitaka mamlaka hiyo (SUMATRA) kupunguza tozo ya faini kwani kutoza faini kubwa siyo kupunguza ajali za barabarani hivyo waige jeshi la polisi la usalama barabarani kwani huwa wanawapa elimu ya barabarani na wanajali thamani ya madereva na wamiliki wa mabasi hayo.
No comments:
Post a Comment