• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 4 January 2018

    Benki kuu yafilisi benki tano nchini

    Benki kuu ya Tanzania (BOT) imezifungia benki tano benki ya Covenant Bank For Women (TANZANIA) Limited,Efatha Bank Limited,Njombe Community Bank Limited,Kagera Famers ' Cooperative Bank Limited na Meru Community Bank Limited  na kusitisha shughuli zote za kibenki,kuzifutia leseni zao zote za biashara za kibenki na kuziweka chini ya ufilisi kutokana na kutotimiza matakwa ya kisheria ya kuwa na mtaji kamili wa kutosha uliowekwa na benki kuu.

    Akizungumza na waandishi wa habari Gavana wa benki kuu ya Tanzania Prof.Benno Ndulu amesema mwaka 2012 benki kuu iliongeza kiwango cha chini cha mtaji wa benki za wananchi (community banks) kuwa shilingi bilioni 2.00 na benki nane zilipewa muda wa miaka mitano ili kuongeza mtaji kufikia kiwango hiko na mda huo uliisha mwezi juni 2017 na muda uliongezwa tena kwa miezi sita hadi tarehe 31  desemba 2017.

    Pia amesema  benki tano  hizo kati ya nane zilishindwa kuandaa na kuwasilisha mpango mkakati unaokubalika wa kuongeza mtaji na kuzifanya benki hizo kuwa endelevu na tayari benki kuu imeteua Bodi ya bima kuwa mfilisi wa benki hizo tano.

    Aidha amesema benki tatu ambazo ni Kilimanjaro Cooperative Bank limited,Tanzania Women's Bank Plc na Tandaimba Community Bank Limited hazikukidhi kiwango cha mtaji na zimewasilisha benki kuu mpango mkakati unaokubalika wa kuongeza mtaji na kuzifanya ziwe endelevu hivyo wamezipa muda wa miezi 6 ili kuweka mtaji na kutekeleza mipango hiyo na endapo zitashindwa kutekeleza zitachukuliwa hatua.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI