• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 3 January 2018

    Wadaiwa sugu elfu 26, wadakwa

    Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo nchini (HESLB),  Abdul Razaq Badru amesema kuwa, kuanzia mwaka jana mpaka sasa wamefanikiwa kuwapata wadaiwa sugu 26,000 wa mikopo ya elimu ya Juu na bado wanaendelea na msako wa kuwatafuta.
    Mkurugenzi huyo amesema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake akielezea namna bodi yake ilivyojipanga kuendelea kuwakabili wadaiwa sugu kwa mwaka 2018.
    Mkurugenzi huyo wa (HESLB) amewapongeza sana waajiri kwa kutoa ushirikiano wao kwa kuendelea kuwasilisha makato ya mishahara kwa waajiriwa wao wanaodaiwa na bodi hiyo kwa asilimia 15 kama sheria inavyosema japo bado kuna waajiri hawajatoa ushirikiano kwani bado hawajaanza kuwakata  kabisa waajiriwa wao.
    Abdul Razaq Badru ameendelea kufafanua kuwa kuanzia Januari nane mwaka huu wataanza kufuatilia taarifa za waajiriwa katika taarifa zao za kibenki ili kubaini nani ni mnufaika wa mkopo ili kuanza kurudisha fedha hizo katika bodi ya mikopo na kuweza kuendelea kunufanisha wahitaji wengine.
    Mpaka sasa bodi ya mikopo inadai jumla ya bilioni 285 kwa wadaiwa  wote, huku mkurugenzi wa bodi hiyo akibainisha kuwa  wanataka kufikia mwezi wa saba wawe na  wastani wa ukusanyaji wa madeni hayo kwa mwezi uwe umefika bilioni 17 kutoka bilioni 13 kama ilivyokuwa awali.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI