Uongozi wa kata ya Nyehunge Wilayani Sengerema mkoani Mwanza, umetolea
ufafanuzi taarifa za kuwepo kwa sheria ya kuwachapa viboko 12 mtu yeyite
atakayekutwa amesimama na mwanafunzi wa kike, na kusema kwamba taarifa
hizo hazina ukweli wowote.
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kuwa uongozi wa kata ya Nyehunge, wilayani Sengerema umepitisha sheria ya kuwachapa viboko 12 au faini ya shilingi 10,000 wanaume wote watakaokutwa wamesimama na wanafunzi wa kike, kufuatia kukithiri kwa tatizo la wanafunzi hao kukatisha masomo kwa sababu ya kupata ujauzito.
No comments:
Post a Comment