Uongozi wa kiwanda cha Urafiki umeanza kuwaondoa kwa nguvu wadaiwa sugu
sambamba na kuchukua mali zao kwaajili ya kufidia malipo ya fedha ya
kodi ya pango wanayodaiwa.
Hilo
limebainishwa leo na Naibu Meneja mkuu kiwanda cha Urafiki Shadrack
Nkelebe, ambaye amesema zoezi hilo linaendeshwa na kampuni ya udalali ya
YONO na tayari wameshawaondoa wapangaji 90 kwa awamu ya kwanza.
Nkelebe amesema awali walitoa siku 14 kwaajili ya wadaiwa hao kuhakikisha wanalipa madeni yao lakini zimeisha bila kufanya utekelezaji hivyo kulazimika kutumia nguvu ili kuwaondoa na kupata fedha za kufidia.
Nkelebe ameongeza kuwa fedha zitakazopatikana zitatumika kwaajili ya kuongeza pato la kiwanda sambamba na kuongeza uzalishaji kwa kutengeneza na kununua vitendea kazi vya kisasa.
Kwa upande wake naibu Mhasibu wa kiwanda hicho Levina Kahwa amesema
wanadai zaidi ya shilingi milioni 600 kwa wapangaji hao lakini tayari
asilimia 60 wameanza kulipa baada ya zoezi hilo kuanza.

No comments:
Post a Comment