• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday, 6 February 2018

    Amdanganya mumewe mjamzito, aiba kichanga

    Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Viongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya wamefanikiwa kumkamata Happy Charles (24) akiwa na mtoto mchanga jinsia ya kike aliyemuiba Hospitali ya Mkoa wa Mbeya hivi karibuni.
    Akizungumza na waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohamed Mpinga, amesema mnamo tarehe 03 Februari mwaka huu, Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo ambaye ni mama lishe aishiye mtaa wa Airport ya zamani jijini Mbeya.

    Kamanda Mpinga amesema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa Mtuhumiwa Happy Charles hapo awali alikuwa akimdanganya mume wake aitwaye Chiluba Peter, ambaye ni Dereva Taxi kuwa ni mjamzito na kwamba amejifungua mtoto wa kike tarehe 31 Februari, 2018.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI