Kuelekea maadhimisho ya siku ya kutokomeza ukeketaji wa wanawake na
watoto wa kike duniani, (FGM) hii leo nchini Tanzania imeelezwa kuwa
kitendo hicho haramu kimepungua na hivyo kutia matumaini.
Bw. Hamad amesema kuwa hata mikoa iliyokuwa inaongoza kwa matukio ya ukeketaji licha ya vitendo hivyo kuendelea lakini vimepungua kwa kiasi kikubwa mpaka kufikia karibu asilimia 50 tofauti na miaka ya nyuma.
Ulimwenguni kote inakadiriwa kuwa wanawake na wasichana milioni 200 wamekumbwa na ukeketaji na hivyo kuwaachia madhara ya kisaikolojia, kiafya na kijamii.
No comments:
Post a Comment