Naibu waziri wa mambo ya ndani ambaye pia ni Mwenyekiti baraza la Taifa la usalama barabarani, mheshimiwa Eng.Hamad Masauni ametoa agizo kwa kampuni zinazouza pikipiki kuacha kuuza pikipiki zilizosajiliwa kwa majina ya kampuni zao hivyo wanapouza wabadilishe umiliki na majina ya wanunuzi yasomeke kwenye kadi kama wamiliki badala ya kampuni.
Amesema hayo Leo wakati akitoa taarifa ya tathmini ya utendaji na utekelezaji wa awamu ya pili ya mpango mkakati wa baraza la Taifa la usalama barabarani wa kupunguza ajali za barabarani kwa asilimia 10% katika kipindi cha miezi sita kuanzia julai - desemba 2017.
Aidha amesema katika awamu ya tatu wanatarajia kuanza kufanya ukaguzi wa magari ya watu binafsi nchi zima kwa kipindi cha miezi miwili utakaoanza tarehe 1/03/2018.
Pia amewataka wamiliki wa magari ya biashara na mizigo ambao magari yao hayajakaguliwa wayapeleke haraka yakaguliwe kwani ifikapo mwezi wa tatu mosi wataanza msalimie mkali wa kuyakamata magari ambayo yatakuwa hayajakaguliwa na kimchukuliwa hatua Kali Kwa mujibu wa sheria.
Sambamba na hayo Mhe.Masauni amesema katika utekelezaji wa mipango ya mikakati yao, baraza limeagiza usimamizi mkali ufanyike katika kudhibiti pikipiki,makosa ya mwendokasi wa magari,madereva walevi,madereva wanayoyapita magari mengine bila kuchukua tahadhali na kubeba abiria na mizigo kupita kiasi na Kwa njia ya hatari.
Pia mpango mkakati wa usimamizi huo utaambatana na utoaji wa elimu Kwa makundi mbalimbali ya watumiaji wa barabara.
..
Friday, 23 February 2018
Habari
No comments:
Post a Comment