Wadau kutoka taasisi mbalimbali hapa nchini wamekutana katika jukwaa la TEHAMA Salama Tanzania (cybersecurity Tanzania (cyberTz) Forum 2018) wakiwa na lengo la kutafakari kwa pamoja mafanikio,changamoto na mwelekeo katika kutekeleza sera ya taifa ya teknolojia ya habari na mawasiliano eneo la usalama.
Akizungumza za na waandishi wa habari kaimu Mkurugenzi Mkuu wa tume ya TEHAMA Samson Mwela amesema hii ni mara ya kwanza jukwaa hilo kukutana na watahakikisha linafanyika si chini ya mara moja Kwa mwaka ili kuweza kubadilishana uzoefu,kutafakari,kutengeneza mikakati ya kukabiliana na changamoto mbalimbali,kuimarisha ushirikiano wa wataalamu na kuweka maazimio ya kuishauri serikali na wadau wengine hatua za kuchukua ili kujenga imani ya jamii katika kutumia huduma za TEHAMA kwa maendeleo.
Pia aliongezea kwa kusema kukutana huko kutawawezesha wao kujipima kwa malalamiko ambayo wananchi wamekuwa wakiyatoa kwa mwaka mzima wameyapatia ufumbuzi ama wameshindwa kuyapatia ufumbuzi.
Aidha amesema baadhi ya changamoto zinazowakabili kutokuwepo na ushirikiano kati ya taasisi na taasisi,uwepo wa maudhui yasiyoendana na maadili ya kitanzania,kusambazwa Kwa taarifa binafsi katika mitandao ya TEHAMA bila ridhaa ya wahusika,wizi na hujuma kwa njia ya mtandao,kupotea kwa taarifa muhimu katika mitandao ya TEHAMA,udukuaji wa taarifa kinyume na taratibu.
Sambamba na hayo amesema kuongezeka Kwa matumizi ya TEHAMA kumeongeza mchango katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini ikiwemo kuwaunganisha wananchi katika maeneo mbalimbali na huduma za fedha na benki japo kuna changamoto kutokana na matumizi yasiyo salama.
Kwa upande wa Mkurugenzi msaidizi wa usalama wa mitandao Steven Wangwe amesema katika mpango huo wa usalama wa mitandao wameanzisha electronic signature ambayo inamtambulisha mtu kiuhalisia mtandaoni na tayari inatumika katika baadhi ya sehemu hapa nchini.
No comments:
Post a Comment