• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday 20 February 2018

    TRA yabaini makubwa Kwa Askofu Kakobe

    Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)imetoa ripoti ya matokeo ya uchunguzi walioufanya kufuatiwa na kauli iliyotolewa na Askofu Zachary kakobe wa kanisa la full gospel bible fellowship katika mahubiri ya ibada ambayo alisema yeye ana pesa kuliko serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

    Akizungumza na wandishi wa habari Kamishna Mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania Charles Kichere amesema askofu Zachary kakobe hana akaunti wala fedha katika taasisi yoyote ya fedha hapa nchini.

    Aidha amesema uchunguzi huo ulibaini kuwa Askofu Kakobe ni mmoja wa wasimamizi wa akaunti za kanisa hilo zilizopo katika benki ya NBC jumla ya shilingi 8,132,100,819.00 ambapo kiasi hiko kimetokana na sadaka,zaka na michango ambayo inatolewa na waumini,hivyo kwa mujibu na sheria hazitozwi kodi.

    Pia wamebaini kanisa hilo halitengenezi hesabu za mapato na matumizi ya fedha ambapo imepelekea matumizi mabaya ya fedha hizo kama vile safari za nje ya nchi ambazo zimedhaniwa na kanisa lakini anasafiri Askofu na familia yake,vilevile  fedha hizo zinatumika kujenga nyumba ya mke wa Askofu kwa jina lake na si kwa jina la kanisa.


    Amesema kanisa lilikwepa kulipa kodi kiasi cha shillingi 20,834,843.00 ambazo zilitokana na uwekezaji Katika makampuni ya kukuza mitaji na lakini kodi hiyo imelipwa baada ya uchunguzi,pia  kampuni inayomilikiwa na Watoto wa askofu huyo ilikwepa kulipa kodi ya sh 37,280,030.00 baada ya uchunguzi walilipa sh 58,114,873.00

    Sambamba na hayo kamishna huyo amesema kanisa linatunza kiasi kikubwa cha fedha kwenye ndoo na majaba ambapo ni kinyume na taratibu za utunzaji wa fedha ,lakini pia uwekaji na utoaji wa fedha hizo  nyingi kutoka benki hawashirikishi vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya usalama wa fedha na wahusika.

    Aidha mamlaka ya mapato Tanzania imetoa wito kwa taasisi zote za dini ambazo zinajihusisha na shughuli zozote za kiuchumi kulipa kodi stahiki na kwa wakati kwa mujibu wa sheria ,kanuni na taratibu za kodi pia amezitaka taasisi hizo kufuata katiba zao ikiwa pamoja na kutengeneza hesabu za mapato na matumiz ya fedha.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI