• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 15 February 2018

    Wanafunzi wenye changamoto za uoni wapewe kipaumbele

    Haki elimu imetoa tafiti ukionyesha wanafunzi wenye changamoto za uoni katika shule jumuishi wanakabiliwa changamoto ikiwemo upungufu wa walimu,fedha za kukidhi mahitaji ya shule,unyanyapaa wa wanafunzi wenye changamoto za uoni kutoka Kwa baadhi ya walimu na wanafunzi wenzao na ubora hafifu wa mazingira ya shule.

    Tafiti hiyo inetolewa leo na Mkurugenzi wa haki elimu John Kalega katika uzinduzi wa taarifa ya matokeo ya utafiti juu ya tathmini ya mafunzo na ushirikishwaji wa wanafunzi wenye changamoto za uoni katika shule jumuishi nchini.

     Pia amesema lengo kuu la utafiti huo ni kutathmini iwapo mazingira ya shule jumuishi (msingi na sekondari) yanakidhi mahitaji ya wanafunzi wenye mahitaji maalum na kama sera na mikakati ya elimu inakidhi mahitaji tofauti ya wanafunzi wakati wa kujifunza na kufundishwa.

    Hata hivyo matokeo ya utafiti huo umejikita katika kuchambua maeneo  makuu matano ambayo ni kutathmini mazingira na vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi wenye changamoto za uoni,usaidizi wa walimu katika kujifunza kwa Watoto wenye changamoto za uoni,namna wanafunzi wenye changamoto za uoni wanapojifunza ujuzi unaohitajika pamoja na ufaulu wao,ushiriki wa wanafunzi wenye changamoto za uoni katika masuala ya kijamii katika shule jumuishi na uelewa wa maafisa elimu juu ya mkakati wa kitaifa juu ya elimu jumuishi.

    Aidha ametoa rai kwa wawakilishi wa serikalini kutoka wizara ya elimu,Tamisemi,taasisi ya elimu,idara,vitengo mbalimbali katika halmashauri,mashirika na taasisi binafsi kushirikiana Kwa pamoja katika kuzitatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wanafunzi wenye changamoto za uoni katika shule jumuishi nchini.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI