Wakulima wa mahindi mkoani Njombe wamedai kuwa bado hawajaanza kuona
manufaa ya kufunguliwa kwa mipaka kutokana na wafanyabiashara kutochukua
mahindi waliyonayo licha ya bei ya zao hilo ikiwa ni chini ya kawaida.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mkoani Njombe wakulima hao wamesema kuwa zao hilo sasa halina soko la uhakika na bei yake imekuwa ni ya chini mpaka shilingi 4500 kwa debe moja la kilo 20 ambazo pamoja na kushuka hakuna mteja anaye fika kununua.
Halmashauri ya wilaya ya Njombe nayo inalalamika kwa kutonunuliwa kwa mazao hayo ambayo ni moja ya chanzo chake cha mapato ambapo awali ilitegemewa wakala wa hifadhi ya chakula (NFRA)
CHANZO EATV
No comments:
Post a Comment