• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 8 February 2018

    Mfumuko wa bei umebaki palepale

    Na Stahmil Mohamed
    Mfumuko wa bei wa Taifa wa mwezi January 2018 umebaki kuwa 4.0%kama ilivyokuwa mwezi Dec 2017.

    Hayo yamezungumzwa leo na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Ephram Kwasigabo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na  takwimu za Mfumuko wa bei ambapo amesema kasi ya mabadiliko ya bei ya bidhaa na huduma kwa mwezi ulioishia jan2018 imekuwa na kasi ilivyokuwa January mwaka Jana.

    Akitaja sababu mbalimbali zilizopelekea Mfumuko wa bei kubaki kama ilivyokuwa kumetokana na bidhaa na huduma  kutokupanda sana na akizitaja baadhi ya bei za bidhaa za vyakula zilizochangia Mfumuko wa bei kufikia asilimia 4.0kati ya mwezi january2017 na january2018 ni pamoja na Mahindi kwa asilimia 8.0,maharage asilimia4.3,Samaki kwa asilimia9.0 na Ndizi za kupika kwa asilimia9.0.

    Aidha Kwasigabo amesema muelekeo wa Mfumuko wa bei ni Sawa na baadhi ya Nchi za Afrika mashariki ikiwemo Uganda ambapo mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi January 2018 umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 3.0kutoka asilimia 3.3kwa mwaka ulioishia mwezi Dec 2017, Kwa upande wa Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi January, 2018 umeongezeka hadi kufikia asilimia 4.83kutoka asilimia4.50kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba 2017.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI