Na Stahmil Mohamed
Mfumuko wa bei wa Taifa wa mwezi January 2018 umebaki kuwa 4.0%kama ilivyokuwa mwezi Dec 2017.
Mfumuko wa bei wa Taifa wa mwezi January 2018 umebaki kuwa 4.0%kama ilivyokuwa mwezi Dec 2017.
Hayo yamezungumzwa leo na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za
Jamii Ephram Kwasigabo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na takwimu za Mfumuko wa bei ambapo amesema kasi ya
mabadiliko ya bei ya bidhaa na huduma kwa mwezi ulioishia jan2018
imekuwa na kasi ilivyokuwa January mwaka Jana.
Akitaja sababu mbalimbali zilizopelekea Mfumuko wa bei
kubaki kama ilivyokuwa kumetokana na bidhaa na huduma kutokupanda sana
na akizitaja baadhi ya bei za bidhaa za vyakula zilizochangia Mfumuko wa
bei kufikia asilimia 4.0kati ya mwezi january2017 na january2018 ni
pamoja na Mahindi kwa asilimia 8.0,maharage asilimia4.3,Samaki kwa
asilimia9.0 na Ndizi za kupika kwa asilimia9.0.
Aidha Kwasigabo amesema muelekeo wa Mfumuko wa bei ni Sawa
na baadhi ya Nchi za Afrika mashariki ikiwemo Uganda ambapo mfumuko wa
bei kwa mwaka ulioishia mwezi January 2018 umepungua kidogo hadi kufikia
asilimia 3.0kutoka asilimia 3.3kwa mwaka ulioishia mwezi Dec 2017, Kwa
upande wa Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi January, 2018
umeongezeka hadi kufikia asilimia 4.83kutoka asilimia4.50kwa mwaka
ulioishia mwezi Desemba 2017.
No comments:
Post a Comment