• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 12 February 2018

    Dulla Mbambe Mwamaso kupima uzito kesho


    NA CHRISTOPHER LISSA
    MABONDIA  Dulla Mbambe na Felix Mwamaso kutoka nchini Malawi, kesho watapima uzito tayari kwa kupanda uringoni Februali 14 mwaka.
    Mahasimu hao watapima uzito katika Hoteli ya National, Keko, jijini Dar es Salaam.
    Mpambano huo unaosubiriwa kwa hamu na wanazi wa masumbwi nchini utapigwa katika Uwanja wa Ndani wa Taifa, jijini Dar e am
    Akizungumza, jijini Dar es Salaam, jana, Mwenyekiti wa Chama cha Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO), Yassin Abdalah ‘Ustadhi’ alisema maandalizi yote yamekamilika ambapo bondia Mwamaso ameingia nchini usiku wa kuamkia leo.
    “Kesho watapima uzito katika hoteli ya National, Keko na Siku ya wapendanao ndiyo siku ya siku pale taifa,”alisema Yassin.
    Aliongeza; “Huu mpambano ni mkubwa kwani watakuwa wanawania ubingwa wa Afrika Mashariki katika uzito wa kilo 76 na utakuwa ni wa round 10,”
    Alisema, mbali na Dulla Mbambe na Mwamaso kupima uzito pia mabondia Mada Maugo na  Jackob Mganga pamoja na mabondia wengine wa mapambano ya utangulizi watapima uzito.
    Mkurugenzi wa Kampuni ya Respect Entertainment, waandaaji wa mpambano huo, Chief  Kiumbe , alisema  utakuwa ni mpambano wa kihistoria.
    “Onyesho litaanza saa 12:00 jioni na litakuwa ni la kisasi, kutokana na mabondia hao kuwa na historia  ya kipekee,”alisema Kiumbe

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI