• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday 13 February 2018

    Waziri mkuu azindua mpango mkakati wa afya nchini

    Waziri Mkuu wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Kassim Majaliwa leo amefanya uzinduzi wa mpango mkakati wa afya moja na dawati la afya moja la uratibu wa afya moja Tanzania uliozihudhuriwa na wadau mbalimbali.

    Akizungumza katika uzinduzi wa mpango mkakati huo Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuzinduliwa Kwa mpango mkakati huo wa afya moja na dawati la uratibu wa afya moja nchini itakuwa chachu ya kuendelea kutambulika kwa dawati hilo na shughuli zake Kwa ujumla na atahakikisha serikali itaendelea kushirikiana na wadau na washirika wa maendeleo ya sekta ya afya katika kuimarisha dawati la afya moja na muundo wake katika kutekeleza mpango wa afya moja Kwa kuijengea uwezo eneo la  uongozi wa afya ili kulifanya dawati hilo kuwa muhimili wa nchi ambao ni muhimu Kwa agenda ya afya duniani.

    Pia amesema serikali ya Tanzania inatambua suala la afya moja kwani ni agenda inayotambuliwa dunia nzima kwani dhana hii inapunguza gharama katika kutishia tishio la magonjwa ya vimelea ambayo hutoka Kwa wanyama kwenda Kwa binadamu hata Kwa mimea pia na kupelekea kusababisha magonjwa ya mlipuko.

    "Dhana ya afya moja inafaa sana katika nchi ambazo zimeendelea na zile ambazo zinakaribiana na maeneo ya wanyama pori kama Tanzania ambako tuna mapori mengi ambayo yameifadhiwa kisheria na mengine yanatunzwa chini ya ngazi ya vijiji na halmashauri za wilaya hivyo kutokana na changamoto hizi tunao umuhimu mkubwa sana wa uzinduzi wa mpango huu ili kulinda afya za wananchi na mimea " alisema Waziri Mkuu.

    Kwa upande wa Waziri wa nchi ofisi ya waziri Mkuu Jenista Mhagama amesema uzinduzi wa dawati hili utaleta msukumo ndani ya ofisi ya waziri Mkuu katika kuhakikisha wanaratibu na kuweka msingi imara wa kuratibu katika sekta zote zinazohusika katika kudhibiti magonjwa nchini na watawajibika Kwa kiasi kinachotakiwa ili kuhakikisha mpango huu kuwa endelevu na utasimamiwa ipasavyo.

    Aliongezea Kwa kusema lengo la uzinduzi huu ni kuimarisha uwezo wa taifa Kwa kuhakikisha kuwa wanaweza kuzuia,kuchunguza na kutahadharisha umma kuhusiana na masuala hatarishi ya kiafya na kupunguza madhara makubwa kupitia mifumo na mipango ambayo itakuwa ni shirikishi ili kuhakikisha taifa linakuwa Salama na magonjwa ya kuambukiza.

    Pia Kwa upande wa Waziri wa maendeleo ya afya,jinsia na Watoto  Ummy Mwalimu amesema uzinduzi huo utarahisisha utekelezaji wa mpango mkakati ambao Wizara ya afya imeiandaa katika kudhibiti magonjwa ya mlipuko nchini na hivyo utaweza kuimarisha afya za wananchi.

    Aidha amesema wanachangamoto katika masuala ya uratibu wa magonjwa ya mlipuko,ukosefu wa chanjo Kwa wanyama ya kuzuia magonjwa na matumizi holela ya dawa Kwa wanyama bila ushauri wa mtaalamu ambao umepelekea usugu wa dawa hivyo mpango huu utaweza kusaidia katika kutatua changamoto hizo.



    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI