Waziri wa fedha nchini Marekani
ameyaonya mataifa yanayoshirikiana kibiashara na Korea Kaskazini kwamba
yanafanya hivyo yakijihatarisha yenyewe.
Akitangaza vikwazo vipya
Steve Mnuchin amesema kuwa kampuni yoyote iliosaidia kufadhili mpango
wa kinyuklia wa Pyeonyang itapoteza haki ya kufanya biashara na
Marekani.Pia aliambia maripota kwamba Marekani sasa huenda ikaanza kupanda na kuchunguza meli zinazo safirisha mizigo Korea Kaskazini.
Vikwazo hivyo vinalenga mabenki na kampuni zinazomiliki meli ambazo Marekani inasema zinafanya biashara na Korea Kaskazini.
Rais Trump alivitaa vikwazo hivyo vizito zaidi, lakini waandishi wanasema kuwa vikwazo kama hhivyo vilivyowekwa hapo awali vililenga mitandao ya kibiashara ya Korea Kaskziniu.
Vikwazo hivyo vinalenga zaidi ya meli 50, kampuni za uchukuzi nchini Korea Kaskazini lakini pia China na Taiwan.
Korea Kaskazini inakabiliwa na vikwazo vya kimataifa pamoja na vile vya Marekani kuhusu mpango wake wa Kinyuklia.
Lakini taifa hilo liliendeleza majaribio ya makombora yake mwaka uliopita ikiwemo majaribio ya silaha za kinyuklia mbali na kombora la masafa marefu linaloweza kufika Marekani.
Marekani inasema kuwa vikwazo hivyo vipya vinalenga kuifinya zaidi Korea Kaskazini ,kupitia kukata vyanzo vyake vya fedha na mafuta ili kutoendeleza mpango wake wa Kinyuklia.
No comments:
Post a Comment