Tuzo hiyo imepokelewa na Mganga mkuu wa serikali prof.Mohamed Bakari wakati wa kikao kilicho wakutanisha wataalamu wa kudhibiti malaria duniani.
Akizingumza Mganga mkuu wa serikali prof. Mohamed Bakari amesema kuwa kikao hicho cha siku mbili kitajadili namna ya kupambana na kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa malaria kwa nchi nzima hasa katika mikoa inaoyoongoza kwa ugonjwa wa huo nchini ikiwemo mikoa ya kanda ya ziwa ambayo ni kigoma, kagera , na geita.
Kwa upande wa meneja mpango wa udhibiti malaria Dokt .Ally Mohamed amesema kuwa serikali ya Tanzania inajivunia kuwa na kiwanda cha kutengeneza vyandarua vyenye dawa,pia ikiwa ni nchi ya kwanza kwa bara la Afrika kutoa vyandarua hivyo ambavyo vinadhibiti maambukizi ya malaria.
Vilevile ameongeza kuwa shirika la Afya duniani (WHO) limeipongeza serikali ya tanzania na wananchi katika hatua ya kudhibiti kuenea Kwa ugonjwa wa malaria na ushirikishwaji wa mzuri katika tafiti walizmbali walizokuwa wanashiriki.
No comments:
Post a Comment