• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday 27 February 2018

    Serikali yadhamiria kuwalinda wasichana dhidi ya magonjwa ya saratani

    Wadau  wa afya  kushirikiana na Wizara ya afya nchini leo wamekutana kwa pamoja kwa lengo la kujadili na kupena taarifa kuhusu chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi sambamba na kupanga mikakati  kwa kiasi gani wanaweza kufanikisha mpango wa utaoji wa chanjo hiyo ndani ya nchi nzima.


    Akiongea katika kikao hiko waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa wanategemea kuzindua rasmi utoaji wa chanjo hiyo ya saratani ya mlango wa kizazi ifikapo Aprili mwaka huu ambapo wasichana walio na umri Kati ya miaka 14-18 watapa chanjo na kuongeza kuwa zitatolewa dozi mbili ambapo dozi ya pili itatolewa baada ya miezi sita Mara baada ya kupata dozi ya kwanza.


    Pia Ummy amesema kuwa chanjo hiyo itagharimu sh.30000 za kitanzania Kwa dozi zote mbili iko moja itagharimu sh.15000 na kuwatoa hofu watanzania kuwa serikali kwa kushirikiana na Wizara ya afya wanahangaika ili kuhakikisha kuwa inafika hatua chanjo hiyo inatolewa bure bila malipo.


    Aidha amebainisha kwamba kwa mwaka huu wamedhamiria kutoa chanjo kwa wasichana 616,734 na kusisitiza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha wanawalinda wasichana wote wenye umri kuanzia miaka 9-14 dhidi ya ugonjwa huo wa saratani ya Shingo ya kizazi na kuongeza kuwa watajitahidi kuwa na takwimu sahihi za watoto wa kike wanaozaliwa ili kuweza kufikia lengo.


    Sambamba na hayo waziri Ummy ametaja maeneo ambayo chanjo hiyo itakuwa inapatikana katika vituo vya afya, baadhi ya shule zitakazochagukiwa na  baadhi ya maeneo ndani ya jamii.


    "Chanjo hii itatolewa kwenye vituo vya afya,  baadhi ya shule zitakazochaguliwa na baadhi ya maeneo yaliyopo ndani ya jamii' amesema Ummy.


    Lakini amewatoa hofu wananchi juu ya chanjo hiyo na kusema kuwa imethibitishwa na WHO kwa kushirikiana na TFDA hapa nchini haina madhara yoyote na inafaa kwa matumizi ya binadamu na kuahidi kwamba ataanzisha kampeni yeye kama mama ili kuhamasisha watu kujitokeza kwa wingi pindi zoezi la utoaji wa chanjo hizo litakapoanza.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI