Wakili Fatma Karume na Mtoto wa aliyekuwa Mbunge Tarime, Chacha Wangwe,
Bob Wangwe wamefunguka na kusema kuwa wamepanga kufungua kesi kupinga
Wakurugenzi kusimamia uchaguzi nchini. Akiongea na waandishi wa habari Fatma Karume amesema kuwa Tanzania
sasa baadhi ya viongozi waliwahi kusikika wakijinadi kushinda uchaguzi
hata kwa magoli ya mkono na kudai kuwa haki ya kura sasa inaonekana kama
haina thamani, hivyo wao wanataka kuipigania haki hiyo kupitia sheria
ili ipatikane.
Aidha Fatma Karume amesema watu ambao waliweka mfumo huo wa
Wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi walikuwa na lengo lao na
walifanya hivyo kwa kuwa walikuwa wanajua nini wanataka kufanya.
"Mtu akipiga kura haina thamani yoyote na matakwa yake
hayasikilizwi kwa sababu kuna kitu kinaitwa goli la mkono, sasa kama
kuna goli la mkono linatoka kwenye mfumo, kama kwenye mfumo kuna refa
anaona, refa wa haki hawezi kukubali goli la mkono lakini tukajiuliza ni
nini kinafanya refa afunge macho au asione watu ambao wanasema wao
watashinda kwa goli la mkono. Kila mtu ana haki ya kupiga kura na kura
yake ihesabike sasa kama kuna watu wanapiga magoli ya mkono haki yako
hii inachukuliwa yaani imetekwa"
"Chini ya Katiba yetu refalii wa masuala haya ni Tume ya
Uchaguzi, Katiba inasema huyo refalii lazima awe mtu ambaye hayumo
kwenye chama chochote cha kisiasa siyo CHADEMA, CCM wala CUF bali
anatakiwa awe mtu ambaye si mwanachama wa chama chochote, kwa hiyo
msimamizi wa uchaguzi ni marufuku kuwa chini ya chama chochote kwa
mujibu wa Katiba yetu yaani kuna matatizo makubwa ya sheria hapa lakini
mwisho unakuta unakuta kwamba wasimamizi wa kura wanavaa magwanda ya
chama siku moja siku ya pili wanavaa sare za sare za Tume ya Uchaguzi
halafu wananchi wanalalamika, na wananchi wanalalamika kwa sababu ya
mfumo na mfumo umewekwa kisheria na watu walioweka huo mfumo wanajua
wamefanya nini" alisema Fatma Karume
Kufuatia mapungufu hayo ya Sheria Fatma Karume amesema kuwa
alichokigundua yeye magoli ya mkono yanatokea kwa sababu ya mfumo na kwa
mfumo huo hizo kura zitapigwa kila siku hivyo ameshauri waende
mahakamani kuhoji mahakama kama mfumo huo unakubalika chini ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inataka kila kura ihesabike, na
katiba inayotaka Demokrasia
No comments:
Post a Comment