• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 28 February 2018

    RC MAKONDA ASHUSHA NEEMA KWA WAFANYABIASHARA WAZAWA DAR

    Katika kutimiza ndoto ya Tanzania ya viwanda ya Rais Dr. John Magufuli mkoa wa Dar es salaam umeweka mkakati kabambe wa kutangaza bure bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali na wafanyabiashara wazawa kupitia Soko la bidhaa zinazozalishwa na wazawa linalotaraji kuanza Mwezi April kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja.

    Huu ni mpango wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kuwakwamua wajasiriamali na wafanyabiashara wazawa kwa kuhakikisha wanamiliki uchumi na kunufaika na uzalishaji wanaoufanya.

    Kwa mantiki hiyo RC Makonda anawaalika wafanyabiashara na Wajasiriamali wote wa Mkoa wa Dar es salaam kukutana na Maafisa Biashara kwaajili ya kuratibu bidhaa walizonazo ili waweze kusaidiwa kutangazwa kupitia Soko la Bidhaa za ndani.

    Hii inawalenga wafanyabiashara wote wa Viwanda vidogovidogo na vikubwa wakiwemo wazalishaji wa Sabuni, Maziwa, Keki, Unga, Nguo, Mapambo, Vyakula, Viatu, Wachojari, Wachonga vinyago na wengineo wengi.

    KUWA MZALENDO KWA KUNUNUA BIDHAA INAYOZALISHWA NA WAZAWA ILI KUKUZA UCHUMI WA TAIFA.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI