ofisi ya tamwimu ya Taifa (NBS) imepiga marufuku kwa shirika lolote kufanya makadirio ya idadi ya watu wa Tanzania na kuchapisha matokeo hayo bila kushirikisha ofisi ya Takwimu kwani kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa sheria ya tawikmu namba 9 .
Akizungumza na waandishi wa habari waziri wa fedha na mipango dokta Philip Mpango wakati wa uzinduzi wa taarifa ya makisio ya idadi ya makisio ya watu katika ukumbi wa Makumbusho jijini dar es salaam amesema makadilo ya idadi ya watu ambayo ayaendani na hali halisi ya watu inaatalisha maendeleo ya nchini.
Pia amesema kasi kubwa ya ongezeko la watu linaleta changamoto ya kuwa na idadi kubwa ya watoto na na vijana ambapo inapelekea kuwa na kiwango cha juu cha watu tegemezi .
"Hivyo serikali imeona katika kukabiliana na changamoto hizo imejieleleza kuwekeza katika elimu na kuhakikisha Mtoto Wa kike anapata fursa sawa ya kusoma na kubakia shuleni pamoja na kutoa elimu bure".Amesema Mpango
Aidha amesema mikakati mingine waliojiwekea ni kuweka msukumo katika ujenzi wa uchumi na viwanda,kutoa fursa sawa kwa wanawake na wanaume kumiliki mali ikiwa pamoja na ardhi na kupanua fursa za upatikanaji wa mikopo na mitaji ili waweze kujikwamua.
Kwa upande wa mkurugenzi mkuu wa ofisi ya takwimu dokta ALBINA CHUWA amesema nchi zote dunani zina utaratibu za kujua idadi ya watu katika vipindi mbali mbali ilikusaidia jamii kuhusu ukuaji wa uchumi nchini.
No comments:
Post a Comment