• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 1 March 2018

    Uchaguzi mdogo siha,kinondoni haukuwa wa haki

    Na Stahmil Mohamed
    Kituo cha sheria na haki za binadamu    kimebaini ukiukwaji wa haki za binadamu katika uchaguzi mdogo wa marudio uliofanyika  SIha na Kinondoni 

    Hayo yamesemwa na kaimu mkurugenzi mtendaji wa kituo cha  sheria na haki za kibinadamu Anna Henga alipokuwa akitoa tathimini ya chaguzi ndogo za Siha na Kinondoni  na kusema kuwa baadhi ya masuala mbalimbali yaliyofanyika katika chaguzi hizo ni pamoja na matumizi ya watoto hasa katika  kutumbuiza katika kampeni uliofanywa na  chama cha mapinduzi makumbusho katika jimbo la kinondoni febr 2 ni ukiukwaji wa haki za kibinadamu hususani haki za watoto,Matumizi ya rasilimali za umma kwa maslahi ya vyama kituo cha sheria na haki za kibinadamu  kimeshughudia viongozi wa serikali wakitumia magari ya umma katika katika mikutano ya kisiasa kinyume na sheria ya vyama vya siasa na sheria za uchaguzi haswa sheria ya gharama za uchaguzi ya mwaka 2010.


    Akiendelea kutaja mambo mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binadamu Bi Henga amesema matumizi ya nguvu  yaliyopelekea baadhi ya watu kujeruhiwa na kuuwa hayo yalitokea eneo la mkwajuni ambapo mwanafunzi wa chuo cha NIT Akwilina Akwilini  Baftah aliuawa kwa kupigwa risasi kufuatia polisi kutumia risasi kuwasambaratisha waandamanaji wa chama cha demokrasia na maendeleo walioandamana kudai viapo vya uwakala katika jimbo la kinondoni sambamba na hilo jeshi la polisi liliendelea kuwashikiria wafuasi 40 wa chadema wakiwemo wanawake wenye watoto wadogo na majeruhi wawili wa risasi .


    Hata hivyo kituo cha sheria na haki za binadamu kimebaini mwitiko mdogo wa wapiga kura kipindi cha uchaguzi ambapo upande wa jimbo la kinondoni idadi ya waliojiandikisha ni 264,055 na watu waliojitokeza kupiga kura ni watu 45,454 sawa na asilimia 17 na kwa upande wa jimbo la siha watu waliojiandikisha ni 55,313 na waliojitokeza kupiga kura ni 32,277 sawa na asilimia 58 hii inafanya idadi ya jumla ya wapiga kura katika majimbo yote kuwa asilimia 24 pekee ya waliojiandikisha,akiendelea kutaja mambo yaliyojitokeza katika uchaguzi  amesema nipamoja na vituo kutokufunguliwa kwa wakati,uwepo wa polisi wengi vituoni,kupotea kwa sanduku la kura,kutokuwepo na usiri wa eneo la kupigia kura hivyo kituo cha sheria na haki za binadamu kimesema kwa changamto hizo mbalimbali zilizojitokeza kinaona uchaguzi ulikuwa huru lakini sio wa haki.


    Aidha bi Henga amesema kwa kutambua uwepo wa changamoto hizo kimeamua kutoa mapendekezo mbalimbali likiwemo Tume ya uchsguzi kuratibu chaguzi mbalimbali kwa kuzingatia sheria taratibu na kanuni zilizopo bila kufungamana na itikadi zozote za vyama vya siasa,Tume ya taifa ya uchaguzi itoe elimu ya mpiga kura ,vyama vya siasa hasa kipindi hasa tawala kuacha matumizi ya rasilimali za umma hasa katika kipindi cha kampeni,vyama vya siasa vijikite kutangaza ilani ya vyama vyao na sio kutumia lugha za kejeli,matusi na vijembe ,kwakufanya hivyo mambo ya ukiukwaji wa haki za binadamu havitakea,pia kituo cha sheria na haki za binadamu kinatambua madhaifu yaliyopo katika sheria zetu za uchaguzi wanapendekeyçza kufanyika kwa maboresho ya sheris na taratibu hizo ili kuboresha chaguzi zijazo ikiwemo wa 2019 na 2028.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI