• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 5 February 2018

    NEC yazungumzia kuhamisha vituo Kinondoni

    Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC imesema uamuzi wa kuhamisha vituo 46 vya kupigia kura katika jimbo la Kinondoni umezingatia matakwa ya kanuni za Uchaguzi kwa kuvishirikisha vyama vyote vya siasa ikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo.
    Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhan Kailima, jijini Dar es Salaam, kufuatia taarifa za  zilizotolewa na baadhi ya magazeti zinazodai kuwa CHADEMA hakikushirikishwa katika uamuzi wa kuhamisha vituo hivyo.
    Bw. Kailima amesema kabla ya uamuzi wa kubadilisha vituo hivyo, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kinondoni aliitisha mkutano na vyama vya siasa tarehe 30 Januari, ambapo wawakilishi 26 wa vyama walishiriki kwenye mkutano huo wakiwemo wawakilishi wa CHADEMA
    Amefafanua kwamba, "kwa mujibu wa kifungu cha 21 (1) cha kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, vituo vya kupigia kura havitakiwi kuwa kwenye maeneo ya watu binafsi, nyumba za mashabiki wa vyama vya siasa au maeneo ya majeshi na ibada".
    Aidha Mkurugenzi huyo ametoa mfano kuwa katika kata ya Kigogo kuna baadhi ya vituo vya kupigia kura vilikuwa ndani ya msikiti wa Kigogo na vingine vilikuwa ndani ya eneo la Zahanati eneo ambalo lilikuwa dogo kutosha kwa ajili vituo vya kupigia kura.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI