Watanzania wametakiwa kuwa na desturi ya kwenda kupima afya zao mara kwa mara ili kusaidia kupata tiba mapema kabla tatizo halijafikia katika hatua mbaya.
Akizungumza Daktari bingwa wa hospitali ya ocean road Dkt.Rosemary Mushi amesema changamoto kubwa wanayokumbana nayo haswa ni kuwatibu wagonjwa wenye saratani kwani asilimia kubwa huwa wanafika wakiwa wamechelewa kupata matibabu.
Sambamba na hayo Dkt.Mushi amesema chanzo kikubwa cha vichochezi vya saratani mfano saratani ya shingo ya uzazi inasababishwa na kirusi kiitwacho HUMANPOPOLEMA pamoja na type ya 16 na 18.
Pia amesema kundi kubwa la vijana linapenda hasa matumizi ya uvutaji bangi,sigara na unywaji pombe ambapo matumizi ya vitu hivyo hupelekea kusababisha saratani ya koo na kusababisha nguvu kazi hasa vijana kuteketea na taifa kukosa nguvu kazi.
Hata hivyo ameiasa jamii kuachana na mila potofu kuhusu ugonjwa wa saratani kwamba hautibiki na kuachana na matumizi mabaya ya vitu vinavyosababisha ugonjwa wa saratani.
No comments:
Post a Comment