Polisi nchini Kenya
wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa
wakijaribu kuishinikiza serikali kuvifungua vyombo vitatu vya habari
nchini vilivyofungiwa kupeperusha matangazo.
"Hii si mara ya kwanza tumiona serikali ya Jubilee ikiangamiza haki za waandishi wa wahabari. Tumeona ikifanyika kwa muda mrefu"
Tom Oketch mmojawapo wa waandalizi wa maaandamano hayo ameiambia BBC .
"Hawa heshimu sheria, hawa heshumi katiba, wananchi wa Kenya hawatawaruhusu kuturidisha katika enzi za Jomo Kenyatta, enzi za Moi, tutapigana nao mpaka mwisho" ameelezea Tom.
Maandamano haya yanajiri wakati viongozi wa upinzani waliokamatwa kwa madai ya kushiriki njama ya kumuapisha kiongozi wa upinzani Raila Odinga kama rais.
Serikali ilizifunga stesheni tatu za televisheni NTV, Citizen na KTN kwa madai kuwa vilipanga kupeperusha moja kwa moja matangazo licha ya onyo kutofanya hivo.
Na sasa makundi ya kutetea haki za kibinadamu, waandishi habari na baadhi ya wananchi wanapanga kufanya maadamano hii leo Nairobi kuishinikiza serikali kutii amri ya mahakama.
No comments:
Post a Comment